News

RAMADHANI BROTHERS WALITEMBELEA HIFADHI YA TAIFA - SERENGETI

​Washindi wa tuzo za American Got Talent, ambao ni wasanii katika mchezo wa sarakasi, Ramadhani Brothers walifikisha tuzo hiyo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti tarehe 07.04.2024 baada ya kuifikisha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro tarehe 03.04.2024 Read More

Posted On: May 11, 2024

KAMPENI YA VOTE NOW ILIWAFIKISHA RAMADHANI BROTHERS JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJRO

​Ramadhan Brothers, vijana wataalam wa sarakasi za “head to head balance” maarufu kama “Ngata” na washindi wa tuzo za America’s Got Talent 2024 walifanikiwa kufika juu ya kilele cha Uhuru mita 5985 kutoka usawa wa bahari, ambacho ndio kilele kirefu zaidi barani Afrika kilichopo juu ya Mlima Kilimanjaro tarehe 03.04.2024. Vijana hao waliamua kupanda mlima kupitia njia ya Marangu safari ambayo iliandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na kampuni ya Utalii ya Zara Advanture. Read More

Posted On: May 11, 2024

BODI YA WADHAMINI TANAPA YAZINDUA OFISI MPYA YA TANAPA KANDA YA KUSINI

Bodi ya wadhamini Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inayoongozwa na Mwenyekiti, Jenerali (Mstaafu) George Waitara , ilizindua Ofisi mpya ya Makao Makuu ya Kanda ya Kusini - TANAPA yaliyopo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya tarehe 28.04.2024. Sherehe hizo za uzinduzi Jenerali Waitara aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya TANAPA, Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Samwel Swedi, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA na viongozi wengine Waandamizi wa Chama na Serikali. Jengo hilo lina jumla ya Ofisi 19, Ukumbi mmoja wa kisasa wa Mikutano wenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 100 na Maktaba moja. Ofisi hiyo imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi millioni 891. Read More

Posted On: Apr 30, 2024

TAARIFA YA MAFANIKIO YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA (2021 – 2024)

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limefanya wasilisho kwa wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina jijini Dar es salaam tarehe 21.03.2024. Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA ndugu Juma Nassoro Kuji alieleza kwa lengo la kuongea na wahariri hao lilikuwa ni kuuhabarisha Umma mafanikio yaliyopatikana katika Hifadhi za Taifa katika kipindi cha miaka mitatu (2021 – 2024) ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita. Read More

Posted On: Mar 21, 2024

MAENDELEO YA UTALII NA MIUNDOMBINU BAADA YA MVUA KUBWA ZA EL NINO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Ngd. Mobhare Matinyi amesema serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inatarajia kujenga barabara za Tabaka gumu ili kuondoa madhara ya uharibufu wa miundombinu hiyo inayotokana na mvua zinazonyesha kila mwaka. Read More

Posted On: Mar 10, 2024

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA OFISI ZA TANAPA MAKAO MAKUU - ARUSHA

​Mkurugenzi wa idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mobhare Matinyi leo tarehe 05.03.2024 ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kukutana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Mussa Juma Kuji, na kisha kufanya kikao kifupi na Menejimenti ya TANAPA jijini, Arusha Read More

Posted On: Mar 06, 2024